Habari

Wasanii wa Tanzania kupata shavu Italy

Baraza la Sanaa la Taifa kuptia wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo limepokea taarifa ya wasanii wa Tanzania kutakiwa kushiriki Maonyesho ya 16 ya sanaa za Kimataifa yatakayofanyika Mjini Rho, Italia kuanzia tarehe 3 hadi 11 Mwezi December 2011.

Kwa mujibu wa katibu mtendaji wa Basata Bwana Materego, maonyesho hayo yatalenga bidhaa za asili na za kiutamaduni kutoka nchi mbalimbali duniani zikiwemo za asili (typical products) , Muziki (Musical events), Ngoma (Dances), Mapambo (colours) na vyakula (flavours) ambazo kwa ujumla wake zinaelezea historia ya nchi na watu wake.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Bwana Materego alisema Baraza linahimiza vyama na mashirikisho ya sanaa, wasanii na wadau wa sanaa kutumia fursa hii kuonyesha kazi mbalimbali za sanaa katika tamasha hilo.

Kwa maelezo zaidi juu ya maonyesho haya, wasanii na wadau wa sanaa watembelee tovuti ya
www.artigianoinfiera.it au kuwasiliana na waandaaji kupitia barua pepe [email protected]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents