Habari

20 Percent: Afande Sele kachanganyikiwa


Uswahiba kati ya wasanii wawili wa Bongo Flava nchini, Afande Sele na 20 Percent umeingia dosari baada ya kutupiana maneno kila mmoja kwa nyakati tofauti kwenye vyombo vya habari.
Maneno hayo yalianza wiki iliyopita baada ya Afande Sele kuzungumza na Clouds FM na kudai kusikitishwa na kitendo cha swahiba wake 20 Percent cha kugoma kutumbuiza kwenye tuzo za muziki za Zanzibar wakati alikuwa amelipwa pesa zote.
Kufuatia mgomo huo, waandaaji walimpeleka lock-up msanii huyo na kubaki na laptop yake mpaka pale atakapowarudishia waandaji hao shilingi milioni moja waliyompa kwaajili ya kuperform kwenye tuzo hizo.
Hatimaye jana 20 Percent alizungumza na kituo hicho cha radio kuhusiana na tukio lenyewe na kusema kuwa Afande Sele amechanganyikiwa na anasumbuliwa na njaa ndio maana anamlaumu.
Akiongea kwa jaziba, 20 Percent amesema Afande Sele ni kama ‘mtoto’ na alimshangaa kufahamu kuwa alifika Zanzibar saa sita usiku bila kuwa sehemu ya kulala kutokana na waandaaji hao kuwa wababaishaji.
Amesema waandaji wa tuzo hizo ni ‘wahuni’ tu ndo maana alikataa kuperform na kuongeza kuwa maisha yake hayategemei muziki wa Bongo Flava.
Kuhusu Laptop yake iliyobaki kwenye mikono ya waandaji wa tuzo hizo, msanii huyo wa ‘Tamaa Mbaya’ amesema hatoifuata Zanzibar bali watampelekea wenyewe.
Miaka ya hivi karibuni, Afande Selena 20 Percent walionekana kuwa maswahiba wa nguvu lakini tukio hilo linaonesha kuutulia doa ushkaji wao.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents