20 Percent: Tanzania kwa sasa hatuna wana muziki bali tuna wana riziki, wanashindana kwenye magari badala ya muziki (+Video)

Msanii na mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva Twety per Cent ameongea kuhusu ujio wake kwenye industry ya Bongo fleva na kuongelea baadhi ya vitu.

@twenty_percent789 percent789 ameeleza kuhusu mabadiliko ya muziki wa Bongo Fleva na kueleza kuwa kwa sasa hakuna wana muziki wa wasanii Tanzania bali kuna Wana Riziki.

@twenty_percent789 percent789 Ameongeza kuwa wengi sio wasanii bali wana force kuishi maisha ya kisanii na ndio mana unasikia watu wengi wakihoji juu ya maisha ya msanii flani mfano gari analotembelea badala ya kuhoji kuhusu muziki wake.

Ameongeza kuwa anashamgazwa sana na wasanii wanaoingia studio kila siku kurekodi na hao ndio wanaoharibu muziki kwa sababu wanaharibu misingi wa muziki.

Pia ameongelea suala la tuzo zilivyoharibiwa baada ya watu kuanza kupeana tuzo kwa kufahamiana.

Pia amemtambulisha msanii wake mpya anayeitwa @Ebldrucula

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW