Habari

Fahamu sababu za Roma Mkatoliki kuuita wimbo wake mpya 2030

Roma20301

Baada ya kukaa kimya kwa zaidi ya mwaka bila kutoa ngoma mpya, hatimaye rapper Roma anatarajia kutoa ngoma yake mpya kesho Ijumaa.

Ngoma hiyo inaitwa 2030 na akielezea maana yake Roma anasema:

Wimbo wangu mpya ambao nimeupa jina la 2030 ama eflu mbili na thelathini maana yake ni hii ni jibu la mathematics nyimbo yangu ya mwisho kutoa ambapo kule tulikuwa tunatafuta thamani ya x na leo hii sasa tumepata x sawa sawa na 2030 yani X=2030, falsafa yake ni kuwa wimbo unamhusu mtoto aliye zaliwa mwaka huu ambao wimbo umetoka 2012 na kwakuwa mapinduzi na changes huanzia nyumbani basi mimi kama Roma nilifanikiwa kupata mtoto wa kiume mwaka huu October 4 na nikamwita Ivan nikiwa na maana ya Gift from God, zawadi kutoka kwa Mungu na kwakuwa miaka ya mtanzania kufikisha umri wa utu uzima ni miaka 18 basi aliyezaliwa leo yani 2012 hadi afikisha umri huo wa miaka 18 basi itakuwa 2030 eflu mbili na kumi na mbili ikijumulisha kumi na nane basi utapata elfu mbili na thelathini (2012+18=2030) na hiyo ndiyo falsafa yake.

Kaa tayari kwa ujio mpya wa Roma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents