Shinda na SIM Account

Video:Meneja mpya Simba SC atema nyongo, ‘tuache fitina’

Hapo jana klabu ya soka ya Simba imelitambulisha benchi lake jipya la ufundi ambapo miongoni mwa walitangazwa ni kocha msaidizi, Irambona Masoud Juma na Meneja mpya wa timu hiyo ambaye ni Richard Robert.

Akizungumza na waandishi wa habari, Richard Robert ameushukuru uongozi wa Simba SC kumpatia nafasi hiyo na kuwata kumpa ushirikiano katika kuhakikisha anasukuma gurudumu la timu hiyo na kusonga mbele .

“Mimi nimekuwa mshabiki wa Simba SC tokea utoto wangu kwa hiyo kusema kweli nimeshukuru sana kupata nafasi ya kusukuma gurudumu hili.”Amesema meneja huyo Richard Robert.

Robert ameongeza “Nashukuru sana viongozi kwa kunipa nafasi hii ninacho waomba ni ushirikiano tu, tupendane, tuache fitina tufanye kazi Simba yetu iyendembele na pia naomba pia ushirikiano kutoka kwenu nyie waandishi wa habari.”

Meneja huyo mpya wa klabu ya Simba, Richard Robert anarithi mikoba ya Dk. Cosmas Kapinga ambaye sasa amerudi kwa muajiri wake.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW