Michezo

Bao lake dhidi ya Arsenal lamfanya Raheem Sterling kuongeza tattoo nyingine mwilini

Nyota wa klabu ya Manchester City, Raheem Sterling amesherehekea bao lake la kwanza msimu huu dhidi ya Arsenal kwakuongeza tattoo nyingine kwenye mwili wake.

Sterling amefunga bao hilo lamapema dakika ya 14 wakati akiikabili Arsenal hapo jana siku ya Jumapili kwenye mchezo wao wa wakwanza wa ligi kuu England.

Kupitia mtandao wake wa Instagram Sterling ameposti picha inayomuonyesha akimpiga kiss mtoto wake Thiago mwenye umri wa mwaka mmoja ambayo ndiyo imetumika katika mchoro huo wa tattoo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 amefanikiwa kupata mtoto mwaka uliyopita kupitia kwa mwanamke wake, Paige Milian. Raheem Sterling sasa anafikisha jumla ya magoli 50 kwenye ligi kuu England baada ya kupata bao hilo lajana siku ya Jumapili dhidi ya Arsenal.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents