Aisee DSTV!

Yanga watangaza kutoshiriki kombe la Kagame 2019, waeleza sababu kubwa 4 za kujitoa

Yanga watangaza kutoshiriki kombe la Kagame 2019, waeleza sababu kubwa 4 za kujitoa

Klabu ya Yanga imetangaza rasmi kuwa haitoshiriki michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati maarufu kama Kombe la Kagame, kwa mwaka 2019.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na  Yanga, imeeleza sababu 4 za kujitoa kwenye michuano hiyo, ikiwemo wachezaji kumaliza mikataba yao na kutokamilika kwa baadhi taratibu za usajili wa wachezaji wapya.

Sababu nyingine ni Kocha wao mkuu Mwinyi Zahera na baadhi ya wachezaji wao kwenda kwenye michuano ya AFCON 2019 nchini Misri.

Mabingwa hao mara 5 wa Kagame, wamejitoa kwenye michuano hiyo ikiwa ni siku chache baada ya wapinzani wao Simba kufanya hivyo.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW