Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

50 Cent aiponda Starz na kuipa tano BET

50 Cent anaonekana kuichukizwa na kituo cha runinga cha Starz ambacho kinaonyesha tamthilia yake ya Power ambayo imefanikiwa kuteka mashabiki wengi.

Rapper huyo ametumia mtandao wa Instagram kukiponda kituo hicho na kukisifia kituo cha runinga cha BET.

“Im starting to think BET is better then STARZ. I don’t want to kiss nobody over there. Now @ConnieOrlando interim head of programming of BET?All day. LOL #50centralbet,” ameandika 50 Cent kwenye mtandao huo.

Hata hivyo kauli hiyo ya msanii huyo inaonekana ni kama kiki kwa kituo cha BET kutokana na hivi karibuni anatarajia kuachia kipindi chake kipya kiitwacho ’50 Central’ kitakachoanza kuruka mwishoni mwa mwezi ujao.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW