Burudani

50 Cent akana mashtaka ya kumpiga ex wake

Jana 50 Cent aliingia mahakamani kwa mara ya kwanza ambapo wakili wake alidai hana hatia katika kesi inayomkabili ya kumpiga mchumba wake wa zamani na mama wa mwanae. Madai mengine ni pamoja na kuharibu mali.

50cent_070313

50 ambaye jina lake halisi ni Curtis Jackson, aliambiwa kukaa mbali na mchumba wake huyo wa zamani Daphne Narvarez na alikatazwa kuwasiliana naye kwa simu ama email. Aliambiwa pia hatakiwi kumiliki silaha na aliambiwa kurejea tena mahakamani Sept. 4.

Narvarez anasema 50 alimshambulia kwenye nyumba yake ya California na kumpiga huku polisi wakisema aliharibu mali yenye thamani ya $7,100.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents