Michezo

50 Cent amwekea Mayweather dau la shilingi bilioni 2.9, anaamini atamchapa Pacquiao

Pamoja na kwamba si marafiki tena, 50 Cent bado anaamini kuwa Floyd Mayweather Jr hapigiki.

50centfloyd

Ndio maana rapper huyo ametangaza kuwa ataweka dau la dola milioni 1.6 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 2.9 kwa bingwa huyo wa masumbwi atakayezichapa na Manny Pacquiao, May 2.

50 na mshikaji wake G-Unit, Tony Yayo alikuwa akizungumza kwenye kipindi cha ‘The Breakfast Club’ ambapo mtangazaji Charlamagne Tha God alipomuuliza anadhani ni nani atashinda kwenye pambano hilo.

“Champ ‘gon smoke em … it’s gonna look like [the fight] was pumped up for no reason,” alijibu 50.

50 anasema alizungumza na Floyd kwenye show ya Chris Brown mwezi uliopita – ikiwa ni mazungumzo ya mara ya kwanza baada ya kipindi kirefu na alidai kuwa Mayweather anajiandaa vya kutosha.

Mwaka jana 50 alimshambulia Mayweather kwenye mitandao ya kijamii ambapo alimtania kuhusu matumizi yake mabaya ya fedha na uwezo wake wa kusoma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents