Burudani

50 Cent atinga Kenya na Somalia kutoa msaada wa bilioni 1

Rapper na mkuu wa kundi la G-Unit kuoka Marekani, Curtis Jackson aka 50 Cent amedondoka pande za Kenya na Somalia kwa ajili ya kutoa misaada mbalimbali ikiwemo maji na chakula.

Kwa mujibu wa World Food Program, 50 Cent ameahidi kusaidia kufikisha saani za chakula bilioni 1 kwa walioathirika na janga la njaa na pia atachangia senti 10 za dola kutoka kwa mauzo ya kila chupa cha kinywaji chake ‘Street King’.

Ujio huu ni baada ya nchi hiyo iliyomo mashariki mwa Africa kukumbumbwa na janga la njaa mwishoni mwa mwaka jana, na kuwaacha mamilioni ikiwemo watoto wakifa kwa ajili ya kukosa maji na chakula.

Msukumo wa rapper huyo umewashtua wengi kwani inasadikika kwamba usalama wa Somalia haujakaa sawa kutokana na ugomvi wa wenyewe kwa wenyewe unaoendlea nchini humo.

Fiddy ameonyesha mfano wa kipekee kujiokeza kutoa mchango wa hali na mali back to his motherland.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents