Burudani

Picha: Historia ya Kara McCullough Miss USA 2017

Usiku wa Jumapili hii, Kara McCullough mwenye umri wa miaka 25 kutoka jimbo la Columbia alitangazwa kuwa Miss USA kwa mwaka huu.

Mrembo huyo alifanikiwa kuliwakilisha jimbo hilo katika mashindano hayo kwa mwaka huu baada ya kutangazwa mshindi wa Columbia mwezi Disemba mwaka jana. Kara alizaliwa katika mji wa Naples, Italy na alilelewa huko Virginia Beach, Virginia nchini Marekani.

McCullough ni mfanyakazi katika kitengo cha US Nuclear Regulatory Commission ambapo alifanikiwa kupata shahada ya kwanza ya sayansi katika Chemistry kwenye chuo kikuu cha South Carolina State University mwaka 2013.


Kara McCullough akiwa ofisini kwake katika kitengo cha US Nuclear Regulatory Commission

Wakati akiwa chuoni hapo Kara alishiriki mashindano ya kumtafuta mrembo wa chuo na kufanikiwa kushinda taji hilo mwaka 2012-2013.

Moja ya ndoto alizokuwa nazo mrembo huyo kwa sasa ni kuhakikisha anawashawishi zaidi watoto ili waweze kupenda kujifunza masomo ya Sayansi, Teknolojia, Engineering na Hisabati. “I love science. I look at this as a great opportunity to … get to experience worldwide culture, as well as just having the opportunity to be impacted by so many children, hopefully in the math and sciences,” alisema Kara wakati alipofanya mahojiano na Refinery29.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents