Burudani

Abdul Kiba asema Sauti za Busara ni zaidi ya darasa

Alikiba na Abdu Kiba ni miongoni mwa wasanii waliotumbuiza kwenye tamasha la mwaka huu la Sauti za Busara linalofanyikia visiwani Zanzibar.

Ali Kiba na Abdul Kiba

Akizungumza na Bongo5, Abdul Kiba amesema ushiriki wao umewafanya kutambua asili ya muziki wa mataifa mbalimbali ya Afrika.

Ali Kiba akifanya yake

“Nimefanya muziki wa band kwenye show nyingi sana lakini Sauti za Busara ni show ya kipekee, ina mvuto wake, kuanzia kwenye asili ya muziki kutoka mataifa mbalimbali ni full darasa,” amesema. “So tumepata experience kubwa sana kuonana na watu wengi ambao ni wa ndani ya nchi na kuangalia nini wanataka katika muziki.”

“Kwahiyo tumeongeza ujuzi mkubwa sana na ningependa hata kuwashauri wasanii wenzangu wajitahidi kufanya live band hata nyimbo zetu tuzirudie kwa njia ya live band kama tulivyoweza kufanya sisi tuzidi kuona mashabiki wetu wanapata burudani ya kweli,” ameongeza.

“Pia tunawashukuru wakazi wa Zanzibar wameweza kutupokea vizuri wale walioandaa tamasha pia wameona show nzuri kwaHiyo tunajivunia kwa hilo.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents