Michezo

Abel Xavier ameteuliwa kuwa kocha mpya wa Msumbiji

Aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Ureno na Liverpool Abel Xavier ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Msumbiji.

0F5563BB00000578-0-image-m-12_1453768860685

Xavier ambaye pia aliwahi kuzichezea timu za Everton na timu ya LA Galaxy ya Marekani alizaliwa nchini Msumbiji lakini akiwa mtoto alielekea nchini Ureno na kulichezea taifa hilo kimataifa.

xavier

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 43 amepewa mkataba wa miaka 2 na ataanza kazi yake tarehe mosi mwezi Februari.

Amepewa jukumu la kuisaidia ‘the Mambas’ ili kufuzu katika michuano ya kombe la bara Afrika mwaka 2017.

Msumbiji iko chini ya kundi H,baada ya kupoteza mechi zake zote mbili kufikia sasa,nyumbani dhidi ya Rwanda na baadaye ugenini nchini Mauritius.

Mechi yake ya kwanza itakuwa dhidi ya Ghana ambao ndio viongozi wa kundi hilo baada ya kushinda mechi zote mbili.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents