Michezo

AC Milan ya uzwa kwa wa China

Kampuni ya China, Rossoneri Sport Investment Lux imekamilisha rasmi ununuzi wa klabu ya AC Milan ya Italia kutoka kwa Silvio Berlusconi kwa Euro milioni 740.

Klabu hiyo ya Serie A imekuwa chini ya umiliki wa bilionea Silvio Berlusconi, tangu mwaka 1986.

Katika kipindi hicho chote, AC Milan ilifaulu kunyakua mataji manane katika ligi kuu na kunyakuwa kombe la vilabu bingwa barani Ulaya mara tano.

Kwa sasa inashikilia nafasi ya 6 katika ligi kuu, alama 20 nyuma ya vinara Juventus.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents