Michezo

AC Milan yatimua kocha nafasi yake kuirithi Gattuso

Klabu ya AC Milan imetangaza kuachana na Kocha wake Mkuu, Vincenzo Montella na nafasi yake kuchukuliwa na Gennaro Gattuso.

Aliyekuwa Kocha wake Mkuu wa AC Milan, Vincenzo Montella

Kibarua cha Montella kilizidi kuwa kigumu wakati timu yake ya Milan ilipokubali kutoka sare dhidi ya Torino siku ya mchezo uliyopigwa hapo jana siku ya Jumapili.

Kablu hiyo yenye maskani yake nchini Itali,imetoa taarifa hiyo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter.

“Milan inatangaza kuachana na Vincenzo Montella kama Kocha Mkuu . Benchi la ufundi lanaimani na Gennaro Gattuso kuziba nafasi ya Montella.” ujumbe ndivyo ulivyosomeka kupitia mtandao wa Twitter.

Gattuso ambaye ni straika wazamani wa Itali na klabu ya AC Milan anarudi kuchukua nafasi hiyo akitokea timu ya Primavera team.

Aliyekuwa Kocha wake Mkuu wa AC Milan, Vincenzo Montella (kushoto) na Gennaro Gattuso (kulia)

Montella ameanza kuitumikia Milan wakati wa majira ya joto mwaka 2016 baada ya kuziongoza klabu za Roma, Catania, Fiorentina na Sampdoria.

Licha ya kupatiwa wachezaji wengi wapya ndani ya kikosi chake na mmiliki wa klabu hiyo, kocha huyo mwenye umri wa 43, amepoteza michezo sita kati ya 11 aliyocheza katika Serie A, na kuiacha ikiwa na alama 20 huku ikishika nafasi ya saba katika msimamo wa ligi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents