Michezo

Achana na Man United, Paul Pogba sasa aipasua bodi ya Barcelona

Bodi ya miamba ya soka nchini Hispania Barcelona imegawanyika juu ya maamuzi ya kuendelea na mchakato wa kutaka kumsajili kiungo wa Manchester United, Paul Pogba kunako dirisha lijalo la usajili mwezi Januari ama kuachana na swala hilo kikubwa ikionekana ni kiwango cha fedha kinachohitajika na mashetani hao wekundu.

Pogba ni miongoni mwa wachezaji watatu wanaowindwa na Barca kwa muda mrefu wakiwemo, Adrien Rabiot wa Paris Saint-Germain na Frenkie de Jong kutoka ndani ya klabu ya Ajax.

Huku pasinashaka Pogba akitarajiwa kuwa mchezaji ghali zaidi kumnunua miongoni mwa hao watatu ambapo ada yake ya uhamisho ikikadiriwa kuwa zaidi ya euro milioni 100 ikiwa ni pamoja na fedha atakazopata wakala wake, Mino Raiola.

Wakati chanzo kimoja cha habari kutoka ndani ya Manchester United kikiiambia tovuti ya ESPN FC kuwa Pogba kamwe hawezi kuuzwa licha ya kuwa na mganyiko baina yake na kocha mkuu Jose Mourinho.

Baadhi ya watu ndani ya Barca wanaamini kumsajili Pogba kutasaidia kupunguza gepu la kibiashara lililoachwa na Neymar aliyetimkia Paris Saint-Germain kwa rekodi ya dunia ya euro milioni 222.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents