Michezo

Achana na Ronaldo na Messi, mfahamu mchezaji huyu hatari anayelitesa bara la Asia (+video)

Ni takribani miaka 10 sasa mchezo wa soka umetawaliwa na miamba miwili ambao ni Cristiano Ronaldo na Lionel Messi huku kila mmoja akichukuwa tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa mara tano.

Lakini tunatakiwa kuwasahau wachezaji hao ,aana kunauwezekano mkubwa wapo wachezaji wenye viwango vikubwa kuliko wao lakini hapo tunaweza kusema wamekosa bahati, narudia tena ndio wamekosa bahati tena mfano mzuri ni kijana Omar Abdulrahman ambaye wengi wamekuwa wakimuita pacha wa David Luiz wa Chelsea kutokana na kufanana kwao.

Utakuwa umeshangaa kusikia jina hilo maana ni geni masikioni kwako, nadhani ulifikiria nitamtaja Neymar, Eden Hazard, Kylian Mbappé, Ousmane Dembélé na wengine ambao majina yao yamezoeleka kusikika kwenye ngoma za masikio yako.

Omar Abdulrahman ni nani?

Huyu ni mmoja kati ya vijana wenye vipaji vikubwa duniani vya soka. Umri wake ni miaka 26 ambapo alizaliwa 20 September, 1991 mjini Riyadh, Saudi Arabia. Ni mmoja kati ya watoto sita katika familia ya mwanasoka wa zamani wa taifa hilo la kiarabu, Abdulrahman Ahmed.

Kijana huyu alianza kucheza soka la mitaani akiwa na umri mdogo sana huko katika mitaa mbali mbali ya Riyadh – Tena alikubalika sana. Katika harakati hizo scout Abdulrahman Eissa, alimwona kwa bahati katika jumba la Al Malaz karibu na uwanja wa Prince Faisal bin Fahd na alifurahi sana kuona kipaji cha mtoto huyo na aliuliza kuhusu klabu ambayo alicheza.

Jibu lilikuwa kwamba hakuwa akicheza kwenye klabu yoyote. Mwaka 2000, alifanya majaribio kwenye timu ya watoto ya Al Hilal ya Saudi Arabia ambapo alifuzu majaribio hayo na kucheza hapo kwa muda wa miaka mitano, lakini dili hilo lilifeli kutokana na ofa iliotoka ilikuwa ikimuhusu Omar peke yake bila kuihusiha familia yake.

baada ya safari ndefu ya kujikita kwenye soka, mwaka 2006 yule scout alimfanyia mipango Omar ya kujiunga na klabu ya Al Ain iliyopo kwenye nchi za Falme za Kiarabu. Al ain walikubali kuwapatia uraia wa huko Omar nd ndugu zake ambapo pia walijiandikisha katika chuo kikuu cha vijana.

Baada ya kujiunga na Al Ain na kupewa uraia wa Falme za Kiarabu

Hapo ndipo safari ya kuteremka mlima kwa Omar ilianza baada ya kuupanda mlima kwa muda mrefu. Alichezea timu ya vijana ya Al Ain kwa misimu miwili (2006-2008) na baadaye alipandishwa kwenye timu ya wakubwa ambapo anacheza mpaka leo.

Lakini pia mwaka 2007 alianza kuitwa kwenye timu ya taifa ya Falme za Kiarabu (UAE) chni ya umri wa miaka 20 ambapo aliichezea mpaka 2010. 2010 mpaka 2012 aliitwa kwenye timu ya vijana ya nchi hiyo chini ya umri wa miaka 23.

Kuanzia mwaka 2011 aliitwa kwenye timu ya taifa ya wakubwa na mpaka sasa ameshaichezea takribani mechi 59 na kufunga mabao tisa.

Kufanya majaribio kwenye timu ya Manchester City

August 6, 2012, Omar Abdulrhamn alithibitisha kupitia mtandao wa Twitter angejiunga na Manchester City ya Uingereza baad aya kufanya majaribio kwenye klabu hiyo kwa muda wa wiki mbili.

Hata hivyo dili hilo lilifeli kutokana na kukosa kibali cha kufanyi kazi nchini Uingereza pamoja na timu yake ya taifa kuwa katika viwango visivyoridhisha kisoka duniani.

Hata hivyo March 9, 2013, kocha mkuu wa klabu ya Al Ain, Cosmin Olaroiu alisema, Man City walimpatia mchezaji huyo ofa ya miaka minne baada ya majaribio na wangerudi tena kumpatia ofa ya pili. March 11, Brian Marwood ambaye alikuwa ni mkuu wa chuo cha Man City, alithibitisha kwamba bado wanavutiwa na Omar.

Wakati huo huo 4 August, 2014 klabu ya Al Ain ilithibitisha kuwa imepata barua ya ofa kutoka Arsenal ambao wanamtaka Omar kwenda kufanya majaribio kwenye timu hiyo, hata hivyo hakuweza kwenda kwenye majaribio hayo.

mafanikio aliyoyapata kwenye soka mpaka sasa

Omar Abdulrhamn amefanikiwa kushinda mataji mengi mpaka sasa ikiwemo manne ya kombe la UAE Pro-League, moja la UAE League Cup, matatu ya UAE Super Cup na matatu ya UAE President’s Cup.

lakini pia ameshashinda tuzo 17 kwenye soka mpaka sasa ikiwemo ya mfungaji bora msimu uliopita, tuzo ya Mars d’Or Arab player of the Year (2015), Asian Footballer of the Year (2016), BA Arab Player of the Year (2016), AGL Emirati Player of the Year (misimu minne mfululizo) na tuzo nyingine.

Mwaka 2015 thamani ya mchezaji huyo ilitajwa kuwa ni kiasi cha paundi milioni 1.3. Tazama hapa chini video ya kiwango cha Omar Abdulrhamn.

https://youtu.be/Z16yd-Q6Bdo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents