Achoma moto Nyumba kwa sababu ya wivu

Grace Simwanza (20) mkazi wa Kilyamatundu huko sumbawanga vijijini hivi karibuni anadaiwa kuchoma nyumba ya familia yake baada ya mumewe kuchukua uamuzi wa kuoa mke wa pili

Grace Simwanza (20) mkazi wa Kilyamatundu huko sumbawanga vijijini hivi karibuni anadaiwa kuchoma nyumba ya familia yake baada ya mumewe kuchukua uamuzi wa kuoa mke wa pili.



Mpaka sasa binti huyo anashikiliwa na polisi mkoani Rukwa akisubiri kufikishwa mahakamani wakati wowote mara tu upelelezi utakapokamilika, ambapo Kamanda wa polisi mkoani humo alisema kuwa mkasa huo ulitokea Jumamosi iliyopita majira ya saa moja usiku wakati mumewe huyo alipokuwa matembezini.



Mwanadada huyo inasemekana alipatwa na ghadhabu baada ya mumewe huyo aliyejulikana kwa jina la Saidi Simba kumwelezea lengo lake la kuoa mke wa pili, jambo ambalo lilimfanya binti huyo kupandwa na ghadhabu na kuamua kumaliza kesi kwa kuchoma nyumba ambayi imepelekea kupatikana kwa hasara ya jumla ya shilingi 340,000.



Aidha kamanda huyo wa mkoani humo aliyejulikana kwa jina la Mantage alifafanua kwa kusema kuwa, Grace alisema ni bora achome nyumba hiyo waliyojenga pamoja n mumewe kuliko kushuhudia mwanamke mwingine anakuja kuitumia wakati kuna jasho lake mule.



“ninachotaka huyu mwananume wangu aanze maisha mapya na huyo mke mdogo anayetaka kumuoa kama ambavyo mimi nilianza naye” alisema Grace alipokuwa akihojiwa na Kamanda wa polisi.



Inadaiwa kuwa siku ya tukio hilo Grace alipatwa na wivu wa hali ya juu alipokaa nyumbani humo mpaka saa saba usiku bila ya kumuona mumewe, moja kwa moja akahisi kuwa atakuwa kwa huyo mwanamke mwengine ambaye ana matarajio ya kumuoa na hapo ndio mwanamama akaamua kuilipua nyumba huku akifikiria anajenga na kumbe badala yake anabomoa.



Pamoja na hayo mwanadada Grace aliweza kukumbuka kutoa vitu vyake muhimu ndani ya nyumba hiyo, wakati moto ulipopamba hakutaka kabisa kupoteza wakati aliamua kukimbia.



Wakati nyumba hiyo inaendelea kuteketea haikujulikana mume wa Grace alikuwa kajichimbia maeneo gani usiku huo ambako alikurupuka na kufika eneo la tukio na kukuta kila kitu kimeteketea kwa moto.


 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents