Habari

ACP Jonathan Shana afariki dunia, Muhimbili waelezea

Aliyewahi kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Jonathan  Shana, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Septemba 16, 2020, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, alikokuwa akipatiwa matibabu.

Akizungumza na EATV mapema leo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano hospitalini hapo Aminiel Aligaesha amethibitisha hilo na kusema kuwa marehemu alikaa hospitalini hapo kwa siku 21 na kati ya hizo alikaa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU), kwa siku tatu.

“Jonathan Shana, Mstaafu RPC Mkoa wa Arusha amefariki usiku wa kuamkia leo Septemba 16, 2020, amelazwa hapa Muhimbili kwa siku 21, na kati ya siku hizo ICU amekaa siku 3”, amesema Aligaesha.

Ikumbukwe kuwa Juni 24 mwaka huu, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, alimhamisha ACP Shana kutoka kuwa RPC na kwenda kuwa afisa mnadhimu shule ya Polisi Moshi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents