Habari

ACT Wazalendo kutikisa na mambo makubwa matano kwa mwaka 2018

Chama cha ACT Wazalendo kimetangaza mambo makubwa matano ambayo ndiyo yatakuwa ndio mwelekeo wao kwa mwaka 2018.

Mhe. Zitto Kabwe

Akitaja mambo hayo Kiongozi wa ACT wazalendo ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Kabwe amesema kuwa ni Kupigania Haki za Wafanyakazi,  Kuongoza juhudi za Ushirikiano na Vyama vingine vya upinzani kwa shabaha ya kuimarisha Demokrasia, Kusemea Haki za Kijamii, kushawishi Sera za Uchumi na Kujikita Katika Uimarishaji wa Chama kwenye ngazi zote na kufanya Mkutano Mkuu wa Chama Mwezi Agosti Jijini Mbeya sambamba na Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia 2018.

Soma na hii – ACT Wazalendo kufanya ziara mikoa 11 

Tayari  Chama cha ACT-Wazalendo kimeanza na jukumu moja wapo kwa kufanya ziara katika mikoa ambayo 11  ili kuimarisha muundo wa Chama hicho kwenye ngazi zote.

Mwelekeo wa Chama cha ACT Wazalendo Katika mwaka 2018

1. Kupigania Haki za Wafanyakazi kupitia Vyama vya Wafanyakazi na haki za raia kupitia vyama vya Wakulima, Wavuvi, Wafugaji na Wafanyabiashara wadogo kwa kujenga ushirikiano wa kipambano na Jumuiya hizo za Wananchi.

2. Kuongoza juhudi za Ushirikiano na Vyama vingine vya upinzani kwa shabaha ya kuimarisha Demokrasia ya vyama vingi nchini kwa kufanya vikao vya Mara kwa Mara na Viongozi wa Vyama vingine na kufanya shughuli za pamoja.

3. Kuendelea kusemea Haki za Kijamii kama Elimu na Afya na kuongeza juhudi za kupigania Haki ya Hifadhi ya Jamii kwa Wananchi wote hasa Wakulima kwa kushawishi kuanzisha Fao la Bei katika mfumo wa Hifadhi ya Jamii nchini na Bima ya Afya kwa kila Mtanzania.

4. Kuendelea kushawishi Sera za Uchumi zinazomkomboa mwananchi wa kawaida kwa kukosoa Sera zinazodidimiza Maendeleo ya Uchumi na kupendekeza Sera mbadala.

5. Kujikita Katika Uimarishaji wa Chama kwenye ngazi zote na kufanya Mkutano Mkuu wa Chama Mwezi Agosti Jijini Mbeya sambamba na Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia 2018.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents