Habari

ACT – Wazalendo walaani mauaji ya watu 250 nchini Somalia

Chama cha ACT – Wazalendo kimeeleza kuwa kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya vifo vya watu zaidi ya 250 vilivyotokea kutokana na mlipuko wa mabomu yaliyokuwa yamewekwa ndani ya lori mjini Mogadishu. Mbali na vifo hivyo, watu zaidi ya 400 wamejeruhiwa katika tukio hilo.

Taarifa iliyotolewa leo  na Mwenyekiti kamati ya mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa, Venance Msebo imetoa pole kwa serikali ya Somalia.

Soma taarifa kamili :

TAARIFA KWA UMMA.
Chama cha ACT Wazalendo kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya vifo vya watu zaidi ya 250 vilivyotokea kutokana na mlipuko wa mabomu yaliyokuwa yamewekwa ndani ya lori mjini Mogadishu. Mbali na vifo hivyo, watu zaidi ya 400 wamejeruhiwa katika tukio hilo. Shambulio hilo linadaiwa kutekelezwa na kikundi cha kigaidi cha Al-Shabab usiku wa jumamosi 14/10/2017.
Inasikitisha sana kuona maisha ya mamia ya watu yakikatizwa kinyama namna hiyo, wakati viongozi, wananchi na taasisi mbalimbali duniani wakifanya juhudi kuhakikisha dunia inakuwa sehemu salama ya kuishi inahuzunisha kushuhudia matukio ya kidhalimu kama hayo yakiendelea kutukia.
Tunatoa pole kwa serikali na wananchi wa Somalia, tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu awajalie uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mamia ya ndugu zao.
Pia tunatoa wito kwa serikali ya, Somalia, serikali ya Tanzania Jumuiya ya Afrika Mashariki, Umoja wa Afrika na jumuiya za kimataifa kuendelea na juhudi za kuleta amani nchini Somalia. Juhudi za makusudi zinapaswa kuchukuliwa ili kuepusha maafa na madhara zaidi yanayoweza kusababishwa na kutokuwepo usalama nchini humo. Somalia isipokuwa salama Afrika haiwezi kuwa salama, bila Somalia salama hakuna dunia salama.
Imetolewa na,
Venance Msebo
Mwenyekiti kamati ya mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa
Dar es salaam 16 Oktoba, 2017

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents