Habari

ACT Wazalendo wasusia kushiriki uchaguzi mdogo wa majimbo matatu, waeleza sababu

Chama cha ACT Wazalendo kimetangaza rasmi kuwa hakitashiriki kwenye Uchaguzi mdogo wa Ubunge wa Majimbo matatu yaliyoachwa wazi.

Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Yeremia Maganja

Akiongea mbele ya Waandishi wa Habari leo Jumapili Desemba 17, 2017, Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Yeremia Maganja amesema wamesusia uchaguzi huo kutokana na ubinywaji wa Demokrasia kwa vyama vya siasa hususani upande wa upinzani na hakuna mazingira ya usawa katika uchaguzi huo.

Ndg Maganja amesema kumekuwa na matukio mengi ya ukamatwaji kiholela kwa viongozi wa vyama vya upinzani bila sababu na vitendo vingine vya dhuruma ambavyo kwa ujumla vinakandamiza uhuru na Demokrasia ya kweli.

Kwa upande mwingine Chama cha ACT Wazalendo kimeshinikiza vyama vingine vya upinzani kususia uchaguzi huo ili kulaani vitendo vya uvunjivu wa demokrasia nchini.

Uchaguzi mdogo wa ubunge wa majimbo matatu ya Loliondo, Songea Mjini na Singida Kaskazini unatarajiwa kufanyika tarehe 13 Januari Mwakani, 2018. Na tayari Chama tawala (CCM) kimeshatangaza washiriki wake katika majimbo hayo.

Soma zaidi–>CCM yampata mrithi wa Lazaro Nyalandu

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents