Habari

ACT – Wazalendo watoa neno Maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar

Chama cha ACT Wazalendo kinawatakia Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla maadhimisho mema ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Taarifa kutoka kwa Chama hicho imeeleza kuwa maadhimisho haya ya Mapinduzi ya Zanzibar yawe kichocheo cha kuimarisha misingi ya undugu.

Soma taarifa kamili;
SALAMU ZA MAPINDUZI KUTOKA ACT WAZALENDO

Chama cha ACT Wazalendo kinawatakia Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla maadhimisho mema ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Maadhimisho haya ya Mapinduzi ya Zanzibar yawe kichocheo cha kuimarisha misingi ya undugu, umoja na mshikamano miongoni mwa Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla.

Kwa Wazazibari, Miaka 54 ya Mapinduzi iwe fursa maridhawa ya kufanya tafakari na tathmini ya kina. Ni kipindi cha kujiuliza maswali. Je malengo ya Mapinduzi ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuleta haki na usawa yamefikiwa? Vipi kuhusu ustawi wa Zanzibar? Ni kwa kiwango gani Mapinduzi ya Zanzibar yameleta maendeleo yaliyokusudiwa ya kiuchumi na kijamii kwa Wazanzibari Wote?

Ujumbe wa Chama chetu kwa Wazanzibar ni kuwa ustawi wa Zanzibar unahitaji jitihada za Wazanziabari Wote bila kujali tofauti za kisiasa. Maadhimisho ya 54 ya Mapinduzi yawakumbushe Wazanzibari umuhimu wa maridhiano ya kisiasa na kuimarisha undugu kwa ajili ya ustawi wa Zanzibar.

Juma Said Sanani, Makamo Mwenyekiti, ACT Wazalendo, Zanzibar.

12 Januari 2018

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents