Habari

ACT Wazalendo watuma barua kwa IGP Sirro

Chama cha ACT Wazalendo kimesema kuwa tayari wametuma barua kwa IGP kuhusu taarifa za tishio la kuuawa kwa Kiongozi wao, Zitto Kabwe.

Akiongea na waandishi wa habari leo kwenye ofisi za chama hiko jijini Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi, Mawasiliano kwa Umma na Uenezi, Ado Shaibu amesema wao wamepokea taarifa hizo kutoka kwenye mitandao ya kijamii.

Katibu huyo ameongeza kuwa hawawezi kupuuzia taarifa hizo kwa kuwa mpaka leo hii bado haifahamiki Ben Saanane yuko wapi.

“Lakini tumemwandikia barua IGP ili achunguze taarifa hizo, hatuwezi kupuuza kwa sababu Chadema ililalamika kabla ya shambulio la Tundu Lissu, hatupuuzi kwa sababu, leo hii hatujui Ben Saanane yuko wapi,” amesema Katibu huyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents