Habari

ACT – Wazalendo wavaa viatu vya wasio na Zahanati wala shule

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amewaomba wanachama wa chama hicho kuchangia shilingi milioni 33 kuchangia huduma za afya na elimu katika Kata zinazoongozwa na madiwani wa chama hicho.

Zitto amesema kuwa gharama za mahitaji yote ni 75.35 Milioni, mpaka sasa kiasi kilichopatikana ni 42.06 Milioni, wanawakaribisha mfuasi wa chama hicho, mwanachama, mwananchi wa kawaida pamoja na mdau wa maendeleo, ili waweze kushiriki kuwezesha upatikanaji wa 33 Milioni zilizobakia.

Kati ya Februari 19 na Marchi 13, Kiongozi wa Chama hicho pamoja na viongozi wenzake, walitembelea kata zinazoongozwa na Madiwani wa Chama hicho.

Changamoto Kuu walizokutana ni Huduma duni za Afya na Elimu (uhaba wa madarasa, zahanati na vituo vya afya). Baada ya ziara, Chama kilifanya tathmini ya mahitaji, ambayo ni mifuko 1,371 ya Saruji (Cement), nguvu kazi hii itatolewa na wakazi wa kata husika pamoja na Mabati 2,680.

Aidha ACT imeeleza kuwa wanatambua kuwa wajibu wa ujenzi huo ni wa Serikali kwa kuwa ndiyo inayokusanya Kodi wao kama chama kupitia falsafa yetu yao ya ‘Siasa ni Maendeleo’ wameona tunao wajibu wa kushiriki kwa vitendo katika mapambano dhidi ya maradhi, ujinga na umasikini hata kama hatuongozi Serikali.

Hata hivyo chama hicho kimeomba kuchangia kiasi chochote kwa aliyenacho kupitia namba ya M-PESA 0744959112 (Jina: ACT Finance)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents