Adam Salamba, Meddie Kagere waing’arisha Simba KAGAME CUP

Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi Simba hii leo kimeendeleza ubabe wake kwenye michuano ya KAGAME baada ya kuwafunga APR ya Rwanda kwa jumla ya mabao 2 – 1.

Wachezaji wa Simba, Adam Salamba aliipatia bao la kwanza timu hiyo dakika ya 72 na kisha Meddie Kagere akitupia dakika ya 90 wakati bao la APR likifanikiwa kufungwa na Nkinzingabo Fiston dakika ya 68.

Kikosi cha Simba kikiongozwa na usajili mpya kama mshambuliaji aliyesajiliwa kutoka Lipuli ya Iringa, Adam Salama na straika, Meddie Kagere kimeonekana kufanya vizuri na hata kukilinganisha na kile cha kwanza kilichotwaa kombe la ligi kuu Tanzania Bara.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW