Burudani ya Michezo Live

Adebayor afikisha klabu ya 10 katika soka, Club Olimpia watangaza kumpa kandarasi

Emmanuel Adebayor amejiunga na Club Olimpia ya nchini Paraguay akiwa mchezaji huru na kutangazwa siku ya Jumanne ya wiki hii.

Emmanuel Adebayor has signed for Paraguayan side Olimpia on a free transfer

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal, Manchester City na Tottenham, Emmanuel Adebayor hii inakuwa klabu yake ya 10 katika ulimwengu wa soka baada ya kumaliza kuitumikia klabu ya Kayserispor ya nchini Uturuki kwa miezi mitatu hadi mwezi Disemba.

Nyota huyo raia wa Togo kwa sasa ana umri wa miaka 35, na kwa muda alihusishwa kujiunga na miamba hiyo ya soka ya nchini Paraguay baada ya rais wa timu hiyo, Marco Trovato kuahidi kumsajili mchezaji huyo.

Olimpia kwa sasa ipo kwenye nafasi ya tano kwenye ligi kuu ya nchi hiyo maarufu kama Apertura ambapo kwa sasa  Adebayor atakuwa pamoja na mshambuliaji wa zamani wa Manchester City, Roque Santa Cruz. Kwa upande wake, Santa Cruz alijiunga na club Olimpia mwaka 2016.

Adebayor will reunite with former Manchester City strike partner Roque Santa Cruz (right)

Klabu 10 alizo zitumikia Adebayor kabla ya kujiunga na Olimpia.

Anajumla ya michezo 446 aliyocheza kwenye ligi mbalimbali, za nchi nne tofauti, Adebayor akifunga jumla ya magoli 161 na ‘assists’52.

2001–2003 Metz, 2003–2006 Monaco, 2006–2009 Arsenal, 2009–2012 Manchester City,  2011 → Real Madrid (loan),  2011–2012 → Tottenham (loan),  2012–2015 Tottenham Hotspur,  2016 Crystal Palace, 2017–2019 Istanbul BaSakSehir,  2019 Kayserispor,  2020– Olimpia

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW