Habari

Adhabu ya Mwalimu Mkuu yasababisha kifo cha mwanafunzi

Mwanafunzi mmoja wa shule ya msingi Matwiga wilayani Chunya mkoani Mbeya, Daudi Kaila, amefariki dunia na mwenzie baada ya kufungiwa kwa muda wa saa mbili na mwalimu wao mkuu kwenye chumba cha hazina ikiwa ni adhabu ya kosa la kutohudhuria shuleni takribani siku tano.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Matwiga, Nehemia Muga amethibitisha kutokea kwa kifo cha mtoto huyo huku walimu wa shule hiyo wakitoroka muda mfupi baada ya tukio hilo kutokea.

Kwa upande wa wanafunzi waliokuwepo shuleni hapo walisema kuwa “Mwalimu akaanza kuita mwanafunzi mmoja mmoja fulani aje hapa, unaulizwa kama huna kosa unaenda kwahiyo hao wawili akawachukua mmoja alikuwa anaomba msamaha akamkatalia akawachukua wanafunzi wawili akasema mpelekeni huko baada ya kuwapeleka kwenye chumba hicho akawafungia na kufuli.”

Matukio mbalimbali ya unyanyasaji wa wanafunzi Mkoani humo yamekuwa yakiendelea baada ya wiki kadhaa kupita mwanafunzi wa Mbeya day kuadhibiwa na walimu kwa kupigwa fimbo mfululizo.

Nikukumbushe kidogo hii video:

https://youtu.be/l2fnEaInIrw

Hata hivyo serikali ya Tanzania iliwachukulia hatua walimu hao.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents