Michezo

Aduana Stars yabanwa mbavu na Raja Casablanca kombe la Shirikisho Afrika

Klabu ya Aduana Stars FC ya nchini Ghana hapo jana imefanikiwa kutoka sare ya mabao 3 – 3 dhidi  ya Raja Casablanca mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika uliyopigwa dimba la Nana Agyemang Badu II Park.

Kwenye mchezo huo mabingwa wa Ghana, mara kadhaa wametoka nyuma na kusawazisha kwenye mchezo huo uliyokwenda hadi dakika 90 kwa sare ya mabao 3 – 3.

Kwenye mechi hiyo iliyokuwa na upinzani wa aina yake mchezaji, Mahmoud Benhalib aliifungia mara mbili Raja kisha Lema Mabidi akatupia la tatu wakati kwa upande wa Stars waliyo iwezesha kutoka sare hiyo ni Oba Ikama, Caleb Amankwah na Nathaniel Asamoah akiisawazishia dakika ya 95 na kuifanya timu hiyo ya kundi A kupata pointi yake ya kwanza baada ya kupigwa 1-0 ugenini dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast.

Michezo mingine ya kombe la Shirikisho la barani Afrika iliyopigwa hapo jana Vita Club 3-1 ASEC Mimosas , Aduana Stars 3-3 Raja Casablanca, UD Songo 0-2 RSB Berkane na CARA Brazzaville 3-0 Enyimba FC , Young Africans 0- 0 Rayon Sports na Gor Mahia 0-0 USM Alger.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents