Habari

Afa kwa kuangukiwa na kontena

Mfanyabiashara mwanamke mkazi wa jijini Arusha, Veronica Paul Odondo (24), amekufa papo hapo baada ya kuangukiwa na kontena lililokuwa limebebwa kwenye lori eneo la Temeke Vetenari, jijini Dar es Salaam.

Na Hellen Mwango



Mfanyabiashara mwanamke mkazi wa jijini Arusha, Veronica Paul Odondo (24), amekufa papo hapo baada ya kuangukiwa na kontena lililokuwa limebebwa kwenye lori eneo la Temeke Vetenari, jijini Dar es Salaam.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, Bw. Emmanuel Kandihabi, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 6:30 mchana.


Kamanda Kandihabi alisema mwanamke huyo aliangukiwa na kontena hilo kati ya mawili yaliyoanguka kutoka kwenye lori wakati akipita kando kando ya barabara.


Kwa mujibu wa Kamanda Kandihabi, lori hilo lenye namba za usajili T 699 AGA, lilikuwa likitoka TAZARA kwenda Bandarini.


Alisema baada ya lori hilo kufika eneo hilo, liliyumba na kumuangukia mwanamke huyo ambaye alikufa pale pale.
Alisema mwili wa marehemu Veronica, umehifadhiwa katika hospitali ya Temeke.


Aidha, alisema dereva wa lori hilo alikimbia baada ya tukio hilo na anatafutwa na polisi.


Katika tukio lingine, moto umeteketeza nyumba yenye vyumba viwili kati ya sita mtaa wa Kanazi, wilayani Kinondoni.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Bw. Jamal Rwambow, alisema chanzo cha moto huo kilitokana na mshumaa.


Kamanda Rwambow alimtaja mmiliki wa nyumba hiyo kuwa ni mfanyabiashara Bi. Mwanaisha Daud (58).


Source: Nipashe

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents