Habari

Afikishwa mahakamani kwa kujifanya msemaji wa Ikulu

Mfanyabiasha Ramadhani Athumani Juma, maarufu kama Elias Jeremiah Mazimbaka amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kujitambulisha kuwa yeye ni Mkurugenzi wa Habari wa Ikulu, Gerson Msigwa.

Amesema hati ya mashtaka jana wakili wa Serikali, Jacqline Nyantori alidai kuwa kati ya Juni 28 na Julai 4,2017 Dar es Salaam kwa nia ya kudanganya alijitambulisha kama Gerson Msigwa ambaye ni Mkurugenzi wa Habari wa Ikulu kwa Ladslaus Matindi.

Amedai kuwa mshtakiwa huyo alifanya kosa hilo katika kipindi hicho kwa lengo la kujaribu kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Mshtakiwa alikana shtaka upande wa mashtaka ulidai upelezi bado haujakamilika. Mshtakiwa ametakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao watasaini bondi ya sh. 1 milioni, kesi imeahirishwa hadi tarehe 23,8,2017 lakini hajakamilisha masharti hayo.

Na Emmy Mwaipopo

Chanzo: Mwananchi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents