Aisee DSTV!

Afisa wa Polisi London ashiriki Big Brother Nigeria bila ruhusa, mashabiki waahidi kumpigia kura za kutosha

Polisi Uingereza immesema kuwa afisa wake Khafi Kareem ambaye ni mzaliwa wa Nigeria anayeishi London alinyimwa ruhusa ya kushiriki kipindi cha televisheni cha Big Brother, lakini alipewa likizo ya bila malipo kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi.

Khafi Kareem in her Met Police uniform, and appearing inside the Big Brother house

Taasisi hiyo ya usalama London imesema hawakubaliani na kitendo cha Khafi kushiriki Big Brother na wala afisa huyo haiwakilishi taasisi hiyo ya usalama. Huku wakisisitiza kuwa afisa yoyote anayekiuka vigezo na masharti ya polisi lazima atawajibishwa.

Hata hivyo msemaji wa afisa huyo ambaye amepamba moto katika mashindano hayo amesema Khafi atajibu atakapoweza. Lakini alilitaka jarida la the sun kufuta habari yake inayosema Khafi anafukuzwa kazi kwa kufanya ngono kwenye kipindi hicho kinacho onyesha Maisha yao halisi katika nyumba ya Big Brother. uku wakiwania kiasi cha pesa cha poundi 68,000.

PC Khafi Kareem attending the Captain Marvel European Premiere held at the Curzon Mayfair, London. Picture date: Wednesday February 27, 2019. Photo credit should read: Ian West/PA Wire

Hata hivyo kitendo cha Polisi London kumkemea Khafi hadharani kimewatibua mashabiki wake ambao wamezidi kuongezeka na kuahidi kumpigia kura ashinde pesa hizo.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha ‘METRO’ Khafi Kareem mwenye umri wa miaka 29, amejiunga na mashindano hayo ya Televisheni mwezi Juni 30 pasipo ruksa ya viongozi wake huku mwanadada huyo akionekana kuwa na kipaji cha uwimbaji na kucheza wakati kwa sasa akikabiliwa na adhabu pindi atakaporejea kazini.

Baadhi ya wanafunzi waliyosoma chuo kimoja na Khafi wamekiambia chombo cha habari cha The Sun kuwa ”Ni ofisa wa Polisi Uingereza, aliomba ruksa lakini alikataliwa. Amefanya kazi hiyo kwa kujitolewa miaka minne kabla ya kuajiriwa rasmi na kuwa ‘constable’ katika kituo cha Lambeth mwaka 2015. Anauwezo wa kuzungumza Kifaransa, Kiitalia na lugha yake ya asili huku akifanya kazi zote za kutafsri (mkalimani).

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW