Habari

Afrika kupata dozi milioni 220 za chanjo ya Corona

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema chanjo ya Covid-19 itakapoaidhinishwa, Afrika itapata karibu dozi milioni 220 za awali.

Breaking News Kiswahili - Afrika kusini kuanza majaribio ya chanjo ya  corona Afrika kusini imeanzisha majaribio ya kwanza ya chanjo ya virusi vya  corona barani Afrika wiki hii, chuo kikuu kinachoongoza hatua

Sehemu ya kwanza ya chanjo hiyo itapewa wafanyakazi wa afya na makundi yaliohatarini, kwa mujibu wa meneja mkuu wa mradi huo katika WHO Afrika, Richard Mihigo.

Amesema usambazaji wa chanjo hizo utategemea idadi ya watu katika kila nchi.

Bwana Mihigo amesema nchi zote 54 barani humo zimeonesha nia ya kutaka chanjo ya Covid-19. Afrika ina zaidi ya watu bilioni 1.3.

Mpango wa chanjo duniani unaofahamika kama COVAX, inakusudia kusaidia kununua na kusambaza kwa usawa dozi bilioni mbili za chanjo zilizoidhinishwa ifikapo mwisho wa mwaka 2021.

Mpango huo una chanjo tisa ambazo zinafanyiwa majaribio duniani

Chanjo mbili kati ya hizo zinafanyiwa majaribio Afrika, kwa mujibu wa mkuu wa muungano wa ubunifu wa maandalizi dhidi ya majanga (CEPI) bwana Richard Hatchett.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents