Michezo

Afya ya Diego Maradona yatia wasiwasi

Afya ya nguli wa soka wa Argentina, Diego Maradona imeonekana kutia mashaka baada ya kuenea kwa kipande cha video katika mitandao ya kijamii kinacho muonyesha gwiji huyo akitembea kwashida wakati wa mazoezi ya timu yake.

Kwa mujibu wa mwanasheria wa Maradona amesema kuwa kutembea kwa kusuasua kwa lejendari huyo wa soka kunatokana na kuchomwa sindano ya kutibu maumivu ya magoti yanayoonekana kumsumbua kwa kipindi chote.

Maradona mwenye umri wa miaka 57, amekuwa akifahamika kusumbuliwa na matatizo ya goti tangu ilivyoripotiwa kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Urusi.

Diego Maradona needs help from No 2 as he limps on to the pitch for Dorados training

Amewahi kwenda Hospitali nchini Colombia kwa matibabu lakini hivi karibuni ameonekana kwenye kipande cha video akiwa anatembea kwa tabu.

Maradona has had injection in his knees previously in order to slow down arthritis effects

Maradona kwa sasa ni meneja wa klabu ya Mexican inashiriki ligi daraja la pili, Dorados lakini kwa mujibu wa kipande hicho cha video kinamuonyesha akitembea kwa shida katika viunga vya timu hiyo huku akipatiwa msaada na kocha msaidizi, Luis Campos.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents