Burudani

Afya ya Tuddy Thomas yaendelea kuimarika

Mtayarishaji wa muziki Tuddy Thomas aliyevamiwa hivi karibuni na vibaka na kukatwa mapanga akiwa nje ya maeneo ya Mlimani City jijini Dar es Salaam, anaendelea vizuri.

11084906_1643712299209962_1817626929_n

Tuddy amesema tayari ameshaanza kufanya mazoezi madogo madogo ili kuimarisha afya yake.

“Naendelea salama ingawa bado sijakaa vizuri, nafanya mazoezi, kwa sababu niliumia mikono yote,” Tuddy alikiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM.

Aliongezea, “Nafikiri mpaka kufika October nitakuwa sawa, nitakuwa nimeanza kufanya kazi. Kazi ndio maisha, pia nimemiss sana kufanya kazi kwa sababu mimi napenda sana kufanya kazi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents