Afya

AFYA: Yafahamu magonjwa manne mapya duniani yanayosababishwa na ngono uzembe, Vijana wapo hatarini zaidi

Kwa sasa duniani magonjwa mapya huibuka kila siku, Na magonjwa mengi ni yale ya kuambukizana na ndio yenye changamoto zaidi kuyakabiri kwa sababu kutokana ya usiri wa waathirika.

Leo tumekuletea bakteria wanne ambao husababisha magonjwa makali mapya ya zinaa ambayo ni tishio kwa afya ya jamii.

1. Neisseria meningitides:
Man starting to take his trousers off

Neisseria Meningitides, pia hufahamika kama meningococcus husababisha uvimbe hatari kwenye uti wa mgongo na ubongo.

Bakteria huyo kwa sasa anapata umaarufu zaidi kwa kusababisha maambukizi kwenye viungo ya uzazi. Kwa mujibu wa Utafiti mmoja uliofanywa miaka ya 1970 ulibainisha baikteria huyo, Kwa namna gani dume moja la sokwe lilivyohamisha bakteria hao hatari kutoka mdomoni na puani kwenda kwenye uume wake baada ya kujilamba sehemu zake nyeti.

Watafiti hao walisema mnyama huyo (sokwe) mara kwa mara hujilamba uume wake na ndio chanzo cha kuanza kusambaa kwa bacteria hao. Utafiti huo ulionesha asilimia 10 ya watu wazima wana bakteria aina ya Neisseria katika makoromeo yao na pua zao.

Tafiti zimebainisha kuwa watu wanaweza kuambukizana bakteria hao kwa njia ya denda au kushiriki mapenzi kwa njia ya mdomo na watu wenye bakteria hao.

2.Mycoplasma genitalium:

Chlamydia infection in a woman's body

Mycoplasma genitalium, moja ya bakteria wadogo zaidi wanaofahamika, wanapata umaarufu mkubwa zaidi ya maumbo yao kwa kusabisha maambukizi hatari ya magonjwa wa zinaa.

Bakteria huyo aligunduliwa miaka ya 1980, Na leo hii anaambukiza asilimia moja mpaka asilimia mbili ya watu duniani hususani vijana.Maambukizi ya Mycoplasma genitalium ambayo kwa kawaida hayana dalili, Wakati mwengine hufanana na dalili za kisonono na kaswende kwa kuwashwa mfululizo kwa mrija wa mkojo kwa wanaume na mlango wa kizazi kwa wanaw
ake.

Bakteria hao kusamabisha maumivu makali ya nyonga kwa wanawake, bakteria huyo anahusishwa pia ugumba, kuharibika kwa mimba, kuzaliwa watoto njiti na hata kufariki watoto tumboni kwa mama.

Ijapokuwa kondomu inaweza kuzuia maambukizi yake, watafiti wanatoa tahadhari juu ya usugu wa bakteria huyo kutibika na dawa za antibaotiki za azithromycin na doxycycline.

3. Shigella flexneri:

Man sitting at the toilet

Shigellosis husababishwa kwa kugusa moja kwa moja au kwa njia moja au nyengine kinyesi cha binadamu. Maambukizi ya bakteria hao hupelekea maumivu makali ya tumbo, na kuhara damu ambapo hustawisha kusambaa kwa bakteria hao.

Ingawaje  ugonjwa huo umekuwa ukionekana zaidi kwa watoto na wasafiri kwenye nchi zenye uchumi mdogo na wa kati, watafiti walianza kupokea visa vya ugonjwa huo kwa wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja toka miaka ya 1970.

Ugonjwa huo, wanasayansi wanaamini, umechukuwa njia mpya ya maamukizi kwa kutumia ngono ya kinyume na maumbile na ngono inayohusanisha midomo na kusabisha maambukizi kadhaa ya gonjwa hilo la zinaa kwa miongo minne sasa.

4:Lymphogranuloma venereum (LGV):

Assorted and colourful condoms

LGV mwanzo hutokea kama kipele ama lengelenge na kisha kushambuli mfumo wa kinga ya mwili na hivyo kupelekea uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi.

Ugonjwa huu pia husababisha maambukizi katika njia ya haja kubwa na pia kusababisha maumivu makali ya tumbo. Katika miaka 10 iliyopita, kumekuwa na maambukizi makubwa ya LGV barani Ulaya na Amerika ya Kaskazini hususani kwa wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Kutumia kondomu kunaweza kupunguza uwezekano wa maambukizi, na kutibu ugonjwa huu kunahitaji walau matibabu ya wiki tatu na kunywa antibaotiki kama doxycycline.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents