Habari

Agizo la Rais Magufuli lamfanya Waziri Jafo kutoa siku 7 kwa wakurugenzi waliochukua mikopo – Video

Agizo la Rais Magufuli lamfanya Waziri Jafo kutoa siku 7 kwa wakurugenzi waliochukua mikopo - Video

Waziri ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Selemani Jafo amezikemea baadhi ya Halmashauri kuendelea kuchukua mikopo kwenye benki za kibiashara kwaajili ya utekelezaji wa miradi yao.

Akizungumza mara baada ya agizo la Rais Magufuli alilolitoa jana akiwa njiani kuelekea Mwanza, ambapo Jafo ametoa wiki moja kuanzia leo hadi Jumatano ijayo apate taarifa ya Halmashauri zote zilizochukua mikopo, kutoka kwenye mabenki kwadhumuni gani na kiasi gani na riba yake ikoje. Aidha Waziri Jafo  hategemei Mkurugenzi yeyote kutoa taarifa za uongo na atakayetoa taarifa za uongo atachukuliwa hatua za kinidhamu. Jafo amesema waliochukua na bado hawajaitumia wazirudishe kwenye mabenki walipokopa na kuanzia sasa kila kitu kisimame.

By Ally Juma.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents