Michezo

Aguero kubaki nje ya uwanja wiki sita

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Manchester City, Sergio Aguero atakuwa nje ya uwanja kwamuda wa mwezi mmoja na wiki mbili baada ya kupata ajali ya gari huko Amsterdam nchini Uholanzi iliyomsababishia kuvunjika mbavu zake hayo yamesemwa na daktari wake.

Taarifa kutoka Manchester City zinasema kuwa kufuatia majeraha aliyonayo mchezaji huyo atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki sita ikiwa ni sawa na mwezi mmoja na wiki mbili daktari, Donato Villani anaamini kuwa huwenda ikamchukuwa muda zaidi.Villani amekiambia chombo cha habari cha TyC Sports “Anajiskia vibaya sana kwasababu anahitaji kucheza lakini kufuatia ajali hii inamkosesha michezo kadhaa.”

“Ataendelea kuwa nje ya uwanja kwa muda wa mwezi mmoja na nusu hatoweza kuondoka mbali na nyumbani kwake ama kupanda gari. Anajiskia vibaya kwasababu anahitaji kuwepo mahala hapa.”

Aguero, ambaye amefunga jumla ya mabao saba katika michezo nane aliyocheza msimu huu ataukosa mchezo wa klabu bingwa barani Ulaya dhidi ya Napoli lakinipia kukosa na Arsenal Novemba 5.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents