MichezoUncategorized

Aguero na kocha wa Bournemouth washinda tuzo ya EPL mwezi January

Mchezaji wa klabu ya soka ya Manchester City, Sergio Aguero amefanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi January katika ligi kuu Uingereza.

Aguero ameshinda tuzo hiyo baada ya kushinda magoli matano katika mechi nne walizocheza. Miongoni mwa magoli aliyofunga mchezaji huyo ni hat-trick yake dhidi ya Newcastle, na mengine mawili akizingu timu za Watford na West Brom.

Wachezaji wengine ambao walikuwa wanawania tuzo hiyo ni pamoja na Kevin De Bruyne, Christian Eriksen, Eden Hazard, Jan Vertonghen na Callum Wilson.

Wakati huo huo, kocha wa Eddie Howe wa klabu ya soka ya Bournemouth amefanikiwa kushinda tuzo ya kocha bora kwa mwezi huo.

Eddie amewabwaga makocha wengine kama Pep Guardiola baada ya kuisaidia timu yake kushinda mechi 4 na kutoa sare 3 zikiwemo mechi mbili dhidi ya Arsenal na Chelsea.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents