Habari

Ahukumiwa kifungo cha miezi 25 jela kwa kuandika CV ya uongo ili kujipatia kazi

Mwanamke mmoja raia wa Australia amefungwa jela baada ya kukutwa na hatia ya kutengeneza CV ya uongo ili apate kazi serikalini ambayo atalipwa mshahara wa dola za kimarekani 185,000 kwa mwaka.

Image result for Australian Veronica Hilda Theriault has pleaded guilty to lying on her resume to land a high-paying government job.

Veronica Hilda Theriault

Veronica Hilda Theriault, mwenye umri wa miaka 45, alishtakiwa mwezi Septemba mwaka 2017 kwa kitendo chake cha udanganyifu.

Dada huyo alifanikiwa na kuajiriwa kwa zaidi ya mwezi mmoja na kujipatia dola za kimarekani 22,500 kabla ya kugundulika na kufukuzwa, hii ni kwa mujibu wa jarida la ABC.

Siku ya Jumanne, Jaji wa mahakama ya Wilaya, Michael Boylan alitoa hukumu kwa Theriault ya kwenda jela kwa muda wa miezi 25 baada ya kukubali makosa yake.

Boylan amesema Theriault aliomba kazi ya Afisa Mkuu wa Habari katika Idara ya Waziri Mkuu na Baraza la Mawaziri (DBC). Maombi hayo ya kazi yalioyokuwa na mashahidi wa uongo, elimu aliyosema na uzoefu wake katika kazi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents