DStv Inogilee!

Airtel Jiunge na Supa 5 yapasua anga Mkoani Dodoma

Huduma ya SUPA 5 imepokelewa kwa shangwe mkoani Dodoma huku dhamira yake
ikiendelea kutimia baada ya umati mkubwa wa vijana kujitokeza ili kufahamu
vyema huduma hiyo nafuu iliyozinduliwa wiki moja iliypota kwa lengo la
kuwapa unafuu wateja wa Airtel ili kufurahia huduma tano nafuu

Wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika tamasha la wazi katika viwanja
vya Barafu mjini Dodoma wasanii wa muziki wa Dansi na Bongo Flaver
walitumbuiza na kufanya tamasha hilo kufana zaidi

Miongoni mwa wasanii waliotumbuiza kwenye utambilisho wa huduma hiyo mpya
kabambe ni pamoja na bendi ya muziki ya mashujaa, kundi la muziki wa kizazi
kipya la Tiptop Connection na kundi la Wanaume TMK.

Akitambilisha huduma hiyo mbele ya wakazi wa mji wa Dodoma na vitongoji
vyake Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando amesema, wateja wa kampuni
hiyo watapata unafuu mkubwa wa gharama za kupiga simu

“Huduma ya SUPA 5 inamuwezesha mteja wa Airtel kutumia mtandao wa facebook
bure masaa 24, kuongea nusu shilingi na watu watatu, kupiga simu kwa robo
shilingi kuanzia saa 4 usiku hadi saa 12 asubuhi na kutumia huduma ya
internet bure usiku kucha” alieleza Bw, Mmbando

Huduma ya SUPA 5 itaendelewa kutambulishwa katika mikoa mbali mbali kwa
kuwa huduma hiyo nafuu ni ya kudumu, mikoa inayotarajiwa kutembelewa kwa
kufanyiwa utambulisho rasmi wa huduma hiyo ya Airtel Supa 5 ni pamoja na
Morogoro, Iringa, Arusha, Mwanza na DSM

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW