Promotion

Airtel na Equity benki yatoa mikopo kwa wafanyabiashara wadogo wadogo Machinga Complex

Meneja Mahusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema kuwa wataendelea na
mikakati ya kusaidia jamii Nyanja mbali mbali za kimaendelea kwa kupitia
huduma ya Airtel Money katika mradi wa upatikanaji wa huduma za kifedha
kupitia simu ya mkononi

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na
Equity bank pamoja na Kampuni ya Ear promotion mwishoni mwa wiki
hii imezindua mradi utakaowawezesha wafanya biashara wadogo wadogo wa soko
la machinga complex jijini Dar es saalam kupata mikopo nafuu kwaajili ya
kuendesha na kukuza biashara zao ambapo mikopo hiyo itatolewa na benki
Equity kwa kupitia huduma ya Airtel money na wao kuwa wakifanya marejesho
ya mikopo hiyo kwa kutumia Airtel money

Akizungumza wakati wa halfa ya uzinduzi wa mradi huo, Meneja uendeshaji wa
benki ya Equity bw, David Mukaru alisema” equity benki iko mstari wa
mbele kuisaidia jamii katika huduma za kibenki ikiwemo mikopo ya riba
nafuu hasa akina mama wa vikundi mbalimbali.

Benki yetu imekuwa sehemu ya maendeleo ya kukuza biashara na mtaji wa
wafanyabiashara wadogo hadi wakubwa nchini. Leo kwa kushirikiana na Airtel
kupitia huduma ya Airtel money tunawawezesha wafanyabiasha wa soko hili la
machinga complex zaidi ya efu tano kupata mikopo ya riba nafuu ambayo kwa
hakika itakuza mitaji na kuwapatia ufanisi zaidi katika biashara zao”.

Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Soko la Machinga Complex, Bw. Abdubakar
Rakesh akizungumza katika uzinduzi wa utakaowawezesha wafanyabiashara
wadogo wadogo wa soko la machinga complex jijini Dar es Salaam. Mpango huo
utawawezesha wamachinga hao kupata mikopo nafuu kwa ajili ua kuendesha na
kukuza biashara zao ambapo benki ya Equity kwa kupitia huduma ya Airtel
Money na wao kuwa wakifanya marejesho ya mikopo hiyo kwa kutumia Airtel
Money

Akiongea kwa niaba ya Airtel Meneja uhusiano wa Airtel bwn Jackson Mmbando
alisema ”Airtel tunaendelea na mikakati yetu ya kusaidia jamii katika
Nyanja mbalimbali za kimaendeleo kwa kupitia huduma ya Airtel money,
katika mradi hu Airtel tunarahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha
kupitia simu yako ya mkononi, tunawawezesha wafanyabiashara hawa kupokea na
kufanya marejesho ya mikopo yao kwa kupitia huduma ya Airtel money”

“Lengo letu Airtel ni kurahisi uendeshaji wa mikopo hii, kuhakikisha
usalama wa fedha, na kupunguza usumbufu wa wafanyabiashara hawa kutembea
umbali mrefu kufanya marejesho ya mikopo hii”. aliongeza Mmbando.

Mkurugenzi wa kampuni ya Ear Promotion ambao wanasimamia na kuratibu mradi
huo, Bw. Brian Kikoti aliwasifu benki ya Equity pamoja na Airtel kwa
kuungana nao katika kusaidia kusimamia ufanisi wa soko la wafanyabiashara
wadogo wadogo

Naye mwenyekiti wa wafanyabisahara wa soko la machinga complex bw.
Abdubakar Rakesh alisema ”ninaishukuru kampuni ya Airtel pamoja na Equity
benki kwa kutufikia sisi wafanya biashara wadogowadogo kwa kupitia mradi
huu wa mikopo nafuu. ni kwa muda mrefu wafanyabiashara wa soko la machinga
complex wamekuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kupata mikopo nafuu
ambayo itawawezesha kukuza mitaji na kuweka bidhaa mbalimbali zitakazo
wavutia wateja kufanya manunuzi katika soko hili, hivyo kwa kupitia mradi
huu tunaamini tutafanikisha matarajio yetu ya kuwa na soko la kisasa lenye
miundo mbinu na hadhi kwa wafanyabishara na wateja wetu.

Umati wa watu waliohudhuria katika uzinduzi wa utakaowawezesha
wafanyabiashara wadogo wadogo wa soko la machinga complex jijini Dar es
Salaam

Naye bw, Brian Kikoti Mkurugenzi wa Ear promotion Kampuni inayosimamia na
kuratibu mradi huo amewasifu Equity Benki pamoja na Airtel kwa kuungana nao
katika kusaidia kusimamia ufanisi wa soko hilo na la wafanyabiashara
wadogowadogo.

Bi. Sara Yohana aliyemwakilisha mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam
akisoma risala katika uzinduzi wa utakaowawezesha wafanyabiashara wadogo
wadogo wa soko la machinga complex jijini Dar es Salaam

Mbali na ushirikiano huu wa kibiashara na Equity bank, Airtel tayari
inashirikiana na mashirika mbalimbali yakiwemo GEPF , LAPF, DAWASCO,
TANESCO, USA EMBASSY, COCACOLA na mengine mengi katika kutoa huduma zao
kupitia huduma ya Airtel money.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents