Promotion

Airtel yaendea kusambaza Mawasiliano Kanda ya ziwa, Mwanza

Mwishoni mwa wiki hii Mwanza Airtel Tanzania imezindua mtambo kabambe
wa mawasilano katika mkoa wa kanda ya Ziwa nje kidogo ya mkoa wa
Mwanza katika wilaya ya Misungwi ikiwa ni mkakati wa Airtel
uliojiwekea katika kuendelea kufikisha huduma zao bora vijijini
Akizindua mnara huo mpya Naibu mwishoni mwa wiki Naibu Waziri Ofisi ya
makamu wa Raisi Mhe, Charles Kitwanga (mawe matatu) amesema Maendeleo
vijijini yatakuwakwa kasi sana iwapo wananchi watatumia mawasiliano ya
simu za mkononi kutafuta masoko ya madini, mifugo au vyakula
wanavyozalisha sehemu mbalimbali
Waziri kitwanga alibainisha hayo katika kijiji cha Nyamayinza kata ya
Gulumungu wilaya ya Misugwi Mkoani Mwanza wakati akiongea na wananchi
na kuzindua mnara wa mawasiliano uliojengwa na kampuni ya Airtel
Tanzania
Alisema “Mawasiliano yanafaida kubwa sana duniani na ndio hufanya
maendeleo ya jamii kwenda kwa kasi, hivyo wananchi wa vijiji vyote
vinavyoizunguka nyamayinza tumieni fulsa ya kupata mawasiliano haya ya
Airtel kwa kuendesha au kuendeleza biashara zenu,pia anzisheni
biashara za kutuma na kupokea pesa za Airtel Money na mtumie
mawasiliano haya haya pia kutafuta wateja wakutosha katika bidhaa za
kilimo na mifugo mnazozalisha”
Nae Meneja mauzo wa Airtel Kanda ya Ziwa Bw, Galus Mgawe akiongea
kwaniaba ya mkurugenzi wa Airtel Tanzania, alisema “Airtel kwa
kukamilisha dhamira yetu ya kutoa mawasiliano yenye uhakika kwa mwaka
huu tunaanza na kuzindua wa mtambo huu wa mawasiliano hapa wilayani
Misungwi utakaowezesha zaidi ya watu 15,000 waliopo vijiji vya
Nyamainza, Buhunda, Ishokela, na Seke kuwasiliana na ndugu na jamaa
kwa uhakika wakiwa Airtel
Kupatikana kwa mtandao huu wa Airtel pia kutasaidia wakazi wa vijiji
vyote na jirani kufurahia huduma zote za Airtel ikiwemo ile ya Airtel
Money, kutuma na kupokea sms, pamoja na kufurahia mtandao bora na
nafuu wa Intaneti.
Uboreshwaji na uwekaji wa Minara ya mawasiliano ya Airtel katika
vijiji unawezeshwa kwa ushirikiano na serikali na mamlaka za
mawasiliano nchini kwa kuwa imetuwekea mikakati bora zaidi wakati wa
uwekaji wa miundo mbinu hii ya mawasiliano kila mahali
Akiongezea kuhusiana na mpango wa kusambaza mtandao unaoendelea
alisema Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw Jackson Mmbando alisema
“kuongezeka kwa mahitaji ya huduma za mawasiliano kutokana na
mazingira au kupanuka kwa shughuli za jamii husika ndio yanayotufanya
Airtel kuitikia wito na kutanua zaidi wigo wa mtandao wetu kwa eneo
husika
“Huduma ya mawasiliano imekuwa moja kati ya nyenzo muhimu katika
kuwezesha shughuli nyingi za kijamii nchini Tanzania na duniani kote,
kupanuka na kufikisha mawasiliano vijijini ni chachu ya kukua kwa
uchumi na kuwezesha jamii iliyopo maeneo hayo kupata miundo mbinu
mbadala katika shughuli za uzalishaji
Airtel bado tunategemea kuendelea kupata ushirikiano wa kutosha kati
yetu na serikali katika kuhakikisha tunafikisha mawasiliano vijijini
kwa kutuwekea mfumo bora wa kulipa kodi na kupata vibali vya kuweka
mitambo ya mawasiliano ili kufaidisha jamii.
Airtel ni mtandao bora ulioenea zaidi na kutoa mawasiliano nchini kote
kwa kufikisha mawasiliano ya uhakikia kwa takribani asilinia 85
kwenye maeneo ya miji na vijiji nchini Tanzania.
-Mwisho-

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents