Promotion

Airtel yagawa vitabu vya milioni 16 kwa sekondari za Dar es Salaam


Mwishoni mwa wiki iliopita kampuni ya simu za mkononi ya airtel imetoa msaada wa vitabu kwa shule za secondary 8 za jijini Dar es Salaam vyenye thamani ya shilingi million 16 ambavyo kwa kiasi kikubwa vitasaidia kuondoa tatizo la upungufu wa vitabu kwa wanafunzi.

Shule ambazo zimebahatika kupata vitabu hivyo ni za jijini Dar es Salaam kutoka wilaya zote zikiwemo Seminary ya Al-Haramain, Whitelake, Mwambao, Hondogo B, Misitu, Yemen, Yeshua pamoja na Archbishop John Sepeku.

Akiongea wakati wa kukabidhi vitabu hivyo wakati hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika shule ya sekondari ya Yemen jijini Dar es Salaam –Temeke Kaimu Afisa Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema kuwa shule nyingi zinakabiliwa na uhaba wa vitabu jambo linalopelekea walimu kuwa na wakati mgumu kipindi cha ufundishaji.

“Ninafurahishwa sana na msaada huu ambao umezifikia shule za mkoa wa Dar es salaam kwa mgawanyo sawa katika wilaya zote kwa kuwa kutokana na uhaba mkubwa wa vitabu pamoja na mahitaji mengine katika shule zetu huwapa walimu changamoto kubwa sana kufikia malengo yao, hivyo bado ninatoa wito kwa taasisi nyingine binafsi na za serikali kuchangia katika elimu kama walivyofanya Airtel Tanzania” alieleza Michael Ole Mugaya.

Naye Meneja wa huduma kwa jamii wa Airtel Hawa Bayumi amesema kuwa Airtel wameguswa na tatizo la ukosefu wa vitabu mashuleni ambao unapelekea kushuka kwa kiwango cha ufaulu katika mitahani ya mwisho. “Vitabu hivi vipo katika mgawanyo sawia katika masomo mbalimbali kama jiografia, hisabati mpaka sayansi. Tunaamini kwamba kila mwanafunzi akiwa na kitabu chake ataweza kuwa makini darasani na baadaye kusaidia kuongeza ufaulu katika mitihani nchini” Alisema Bi. Hawa Bayumi.

Akizungumza kwa niaba ya waalimu wenzake wa shule zilizofaidika na mradi huo Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Yemen iliyopo Dar Es Salaam, alisema kwamba wamefurashwa sana na mradi huo wa kijamii wa Airtel wa kugawa vitabu na kwamba huo ni msaada mkubwa sana katika shule zao “tunawashukuru sana Airtel kwa msaada wenu huu ambao lengo lake ni kufikia malengo ambayo sisi waalim tumejiwekea katika shule zetu ili kuboresha kiwango cha elimu kwa wanafunzi tunaowafundisha tunawaahidi kuvitunza ili vitumike kwa muda mrefu alimaliza kwa kusema Mkuu wa sekondari Yemen…”

Airtel kupitia mradi wake wa ‘Airtel shule yetu’ zaidi ya shule 93 za sekondari zinatarajia kunufaika na mradi wa unaolenga kugawa Vitabu na vifaa vingine vya kujifunzia kwa shule za sekondari nchini mwaka huu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents