Promotion

Airtel yakabidhi gari kwa mshindi wa Yatosha Zaidi Mtwara mwishoni mwa wiki

Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel imekabidhi Gari aina ya Toyota IST kwa mshindi wa Tatu wa droo ya kwanza Promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi inayofanyika kwa kipindi cha miezi mitatu ambapo jumla ya magari 60 yatatolewa kwa wateja wanaotumia mtandao huo.

pic 4
Mkuu wa wilaya ya mtwara Mh, Wilman Kapenjama akimpongeza mzee Sefu Namtapika (60) baada ya kumkabidhi gari yake aina ya Toyota IST mpya aliyojishindia kupitia promosheni ya Airtel Yatosha zaidi na kukabidhiwa katika viwanja vya Mashujaa mkoani Mtwara mwishoni mwa wiki hii

Gari hilo la tatu limetolea kwa mshindi kutoka mkoani Mtwara ambaye ni mwalim mstaafu Seif Namtapika Katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya mashujaa. Namtapika amesema hakuweza kuamini mpaka hapo alipouliza katika ofisi za Airtel za mkoani hapo.

pic 6

“Ndugu zangu sikuamini kabisa nilipopigiwa kuambiwa nimeshinda, wala nilikuwa sijui kama kuna siku ntamiliki gari na tena ukizingatia mimi nimeshastaafu, kweli nawashukuru Airtel pamoja na mungu wangu kwa kunipa zawadi hii” alisema Namtapika.

pic 8
Mkuu wa wilaya ya Mtwara Wilman Kapenjama akikabidi funguo ya gari kwa Mshindi wa Promosheni Airtel yatosha Zaidi mkoani Mtwara bw, Sefu Namtapika (60) ambae ni mwalimu mstaafu aliyeibuka na ushindi wa Toyota IST kupitia droo ya kwanza ya promosheni Yatosha zaidi inayoendesha na Airtel. Wanaoshuhudia makabidhiano hayo ni toka kushoto nyuma ni Meneja mauzo wa Airtel mkoa wa Mtwara Bw, Batlomeo Masatu, Afisa Masoko wa Airtel Bi Aminata Keita, na Meneja Biashara wa kanda ya Pwani Albert Majuva

Naye mkuu wa wilaya ya Mtwara, Willman Ndile Kapenjama aliyehudhuria hafla ya makabidhiano ya gari hiyo iliyofanyika viwanja vya mashujaa Mtwara alisema, “hii ni njia bora kwa kampuni ya Airtel kurudisha faida kwa wananchii ambao kwa kiasi kikubwa wanatumia mtandao huo na ninawasihi endeeni kushirikiana na jamii kwa kila njia ili kubadilisha maisha na ndoto za wateja wengi.”

pic 9
Meneja Biashara wa kanda ya Pwani Albert Majuva (wakwanza kulia) akimpongeza Mshindi wa Promosheni ya Airtel yatosha Zaidi mkoani Mtwara Sefu Namtapika ambaye ni mwalimu mstaafu aliyeibuka na ushindi wa Toyota IST kupitia droo ya kwanza ya promosheni Yatosha zaidi inayoendesha na Airtel. Anayefuata ni Afisa Masoko wa Airtel Bi Aminata Keita na Meneja mauzo wa Airtel mkoa wa Mtwara Bw, Batlomeo Masatu wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika mkoani humo kwenye viwanja vya mashujaa mwishoni mwa wiki

Naye mkuu wa Mauzo wa kanda ya kusini Albert Majuva anasema imekuwa faraja kwa mshindi kutoka katika kanda ya kusini kutokana na wananchii waliowengi kutumia mtandao wa Airtel.

pic 10
Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akiongoza umati wa wakazi wa mkoani mtwara waliojitokeza katika viwanja vya Mashujaa kushudia hafla ya makabidhiano ya gari Toyota IST kwa mshindi wa droo ya kwanza ya promosheni ya Airtel Yatosha

Promosheni hiyo ya Airtel yatosha zaidi inafanyika kwa kipindi cha miezi mitatu ambapo inampa Fursa mtumiaji wa Airtel kujipatia muda wa maongezi zaidi,idadi SMS zaidi na kumpa mteja Internet zaidi kwa ajili ya kuperuzi awapo mahali popote na vile vile kutoa nafasi kwa mteja mmoja kujishindia TOYOTA IST moja kila siku kwa muda wa miezi miwili.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents