Promotion

Airtel yatoa msaada wa vitabu shule ya secondary Mtipa wilaya ya Singida Mjini

Airtel Tanzania kampuni ya simu za mkononi yenye kutoa huduma bora
nchini kote, leo imetoa msaada wa vitabu katika shule ya sekondari
Mpita ikiwa ni sehumu ya shughuli zao za kusaidia jamii.
Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki katika ofisi za Airtel
mjini Dar Es Salam kwa ajili ya shule ya sekondari ya Mtipa wilaya ya
Singida mjini. Mwawakilishi wa shule hiyo ambaye ni mzawa wa eneo hilo
bi Mary Hiki alikabidhiwa msaada huo wa vitabu na Meneja wa huduma
kwa Jamii wa Airtel, Bi Hawa Bayuni. Shule imepewa msaada wa vitabu
vyenye thamani ya shilling milioni mbili.
Vitabu vilivyotolewa ni pamoja na Hisabati, Phisikia, Biolojia,
Kiswahili. ambapo vimekuwa na uhitaji mkubwa shuleni hapo.
Akiongea wakati wa makabithiano hayo yaliyofanyika katika ofisi za
Airtel mjini Dar Es Salaam Meneja Huduma kwa jamii wa Airtel Tanzania
Hawa Bayuni alisema” Airtel kwa kupitia kampeni yake ya kusaidia
jamii imeweza kuwafikia wanafunzi wengi na shule nyingi nchini
Tanzania na leo tunafurahi kuwa sehemu ya maendeleo ya shule ya
sekondari wilayani Singida na kuweza kuchangia vitabu zitakavyotumika
katika kufundishia na kuwa nyenzo muhimu kwa walimu na wanafunzi wa
shule hii Tutaendelea kushirikiana na Serikali chini ya Wizara ya
Elimu katika kuinuia na kuboresha kiwango cha elimu nchini kwani
tunatambua elimu ndio ufunguo wa maisha na vijana ndio nguvukazi ya
kesho. Aliongeza Bayuni.
Mwakilishi wa Shule hiyo bi Mary Hiki mzawa wa Singida alisema tunayo
fuhara kuona Airtel inajito katika kusaidia kuinua kiwango cha elimu
nchini, moja kati mikakati ya elimu halmashauri yetu iliyojiwekea ni
kuhakikisha kwamba kila nyumba moja ya mkazi wa Singida anatoka
graduate na ili kufikia malengo yake kuna mahitaji makubwa ya vitabu
vya kufindishia, tunashukuru sana Airtel kwa kutusaidia katika
kutimiza malengo tuliojiwekea.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imekuwa ikitoa misaada mbalimbali
kama vile Vitabu vya shule ya sekondari, mwezi uliopita Airtel ilitoa
msaada wa kutoa computer 4 na Vitabu vyenye dhamani ya millioni tano
kwa shule ya sekondari Mazombe iliyokokilomita nne kutika Iringa mjini
. Hii ikiwa nikatika kurudisha faida inayoipata na kuchangia katika
huduma kwa jamii.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents