Promotion

Airtel yatoa msaada wa vitabu shule ya sekondari Kisawasawa Kilombero- Morogoro

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kwa kupitia mpango wake
wa ‘Airtel shule yetu’ imetoa vitabu vya ziada na kiada kwa shule ya
sekondari Kisawasawa ya mkoani Morogoro lengo likiwa ni kusaidia
maendeleo ya elimu mkoani hapo na kutoa huduma kwa jamii.

Hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika shule ya sekondari
Kisawasawa na kuhudhuriwa na wawakilishi wa shule, wanafunzi,
waandishi wa habari na wafanyakazi wa Airtel ambapo vitabu vyenye
thamani ya shilingi milioni mbili vilikabidhiwa kwa shule hiyo.

Akiongea wakati wa halfa ya makabidhiano ya vitabu hivyo, Afisa
Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki alisema, ” Airtel
inatambua kuwepo kwa uhaba wa vitabu na vifaa vya kufundishia katika
shule zetu na katika kutatua changamoto hizo tunaongeza nguvu na
kushirikiana na Serikali chini ya wizara ya elimu kuweza kuinua sekta
ya elimu.

“Tunafahamu umuhimu wa elimu katika kujikwamua na umaskini, hali ngumu
ya maisha na kupata nguvu kazi ya kesho, kwa kutoa kipaumbele kwa
kusaidia na kuhakikisha nyenzo muhimu za kufandishia zinapatikana
mashuleni ili kuweza kufikia dhamira yetu ya kusaidia jamii kwa ujumla
Airtel inatoa fulsa sawa kwa shule zote nchini na leo tumewafikia
wanafunzi wa Kisawasawa Kilombero Morogoro. Tunaamini elimu ndio
ufunguo wa maisha hivyo tunayo malengo ya dhati kabisa katika kusaidia
kuinua kiwango cha elimu.

Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari ya Kisawasawa bw,
Menasi Msigwa ameishukuru Airtel kwa kuwawezesha kupata vitendea
kazi na kuongeza kuwa shule hiyo bado inakabiliwa na changamoto
nyingi katika elimu hivyo kuiomba kampuni hiyo kuendelea kuisaidia
katika mambo mengine.

Aidha alichukua fulsa hiyo kuwaasa wanafunzi kutumia na kuvitunza
vitabu hivyo ili viweze kusomwa na wanafunzi wengi zaidi na kuongeza
kiwango cha kufaulu katika shule hiyo
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imekuwa ikitoa misaada mbalimbali
kama vile Vitabu vya shule ya sekondari, wiki iliyopita Airtel ilitoa
msaada wa Vitabu kwa shule ya Mtipwa iliyopo mkoa wa Singida.
Tangu Airtel ilipoanza mpango wa kusaidia vitabu kwa shule mbali mbali
za sekondari hapa nchini, takribani miaka saba iliyopita,
imeshazifikia zaidi ya shule za sekondari tofauti zipatazo 1,000
nchini Hii ikiwa nikatika kurudisha faida inayoipata na kuchangia
katika huduma kwa jamii.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents