Promotion

Airtel yatunukiwa cheti cha heshima kwa udhamini wa wiki ya Nenda kwa Usalama

Kampuni ya mtandao wa simu ya Airtel Tanzania imetunukiwa cheti cha heshima kwa kuwa wachangiaji, wazuri katika kampeni ya kupambana na kupunguza ajali barabarani pamoja na wiki ya Nenda kwa Usalama kitaifa inayoadhimishwa rasmi katika Mkoa wa Iringa.

Airtel imekabidhiwa cheti hicho na wizara ya mambo ya ndani kupitia kitengo cha trafiki.

Makabidhiano hayo yalifanyika jana katika ufunguzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa mkoani Iringa ambapo Meneja wa Airtel Kanda za Nyanda za Juu Kusini, Beda Kinunda aliiwakilisha kampuni hiyo katika kupokea cheti hicho.

Wakati huo huo Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mbando alimkabidhi Moderm ya Airtel 3.75G Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo ya Simu ambao ni wadhamini wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa inayofanyika mkoani Iringa.

Airtel Ni mmoja wa wadhamini waliofanikisha sherehe hizo za uzinduzi huo.

Angalia picha za uzinduzi huo wa wiki ya nenda kwa usalama kitaifa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents