Promotion

Airtel yazindua minara inayotumia solar vijijini


Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa kutoa huduma zenye wigo
mpana zaidi imezindua minara yake inayotumia Umeme unao tumia nguvu za
nishati ya Jua katika kijiji cha kimande kata ya itunguru mkoani Iringa.
Uzinduzi huo ni moja kati ya mikakati ya Airtel kuhakikisha inaendeleza
mipango yake ya kupanua upatikanaji wa mawasiliano katika maeneo mbalimbali
nchini kirahisi, kupunguza gharama za uendeshaji na kuhamasisha utunzaji wa
mazingira katika maeneo yenye minara yake nchini.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo Mwenyekiti wa kijiji cha Kimande kata ya
Itunungu Tarafa ya Pawaga Iringa Vijijini Bw, Andason Mpululu ameushukuuru
uongozi wa Airtel kwa kuweza kukabili changamoto za mawasiliano kijijini
hapo na kuwa sehemu ya uboreshaji wa uendeshaji wa biashara mbalimbali hasa
za kilimo cha mpunga ambapo hapo awali upatikanaji wa soko ulikuwa mgumu
sana kutokana na kutokua na mawasiliano thabiti kama ilivyo sasa.

“Kwa kupitia Mtandao na huduma ya Airtel money huduma za kifedha
zimeboreshwa, zimekua karibu zaidi na kuwawezesha wafanyabiashara kupokea
malipo ya bidhaa zao kirahisi, kwa gharama nafuu na bila usumbufu wowote.
Nimatumaini yetu kuwa kwa kupitia umeme wa sola gharama za mawasiliano ya
simu za mkononi yataaendelea kupungua na kuboreshwa zaidi na kuleta tija kwa
wananchi hasa wenye kipato kidogo,”alisema bwa Mpululu.

Naye mkazi wa kata ya Itunungu bwana Jumanne Zuberi alisema, “tunashukuru
sana serikali kuwawezesha wawekezaji kuwekeza katika sekta ya mawasiliano na
hivyo kufikiwa na mtandao wa Airtel. Hapo zamani upatikanaji wa mawasiliano
ulikuwa ni changamoto kubwa hivyo kuwafanya wakazi wa kijiji hapa kutembea
umbali mrefu kupata mawasiliano. Tunashukuru kwa sasa huduma za simu kijini
hapa zimeweza kuboresha shughuli mbalimbali za kiuchumi, kijamii na
kuboresha usalama wa raia na mali zetu.”

Akiongea kwa niaba ya kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Meneja Uhusiano
bw, Jackson Mmbando alisema, “nia yetu ni kubadili matumizi ya mafuta ya
diesel na generator kuendesha mitambo yetu ya mawasiliano na kutumia umeme
wa nishati ya jua ambao utasaidia katika kutunza mazingira na kupunguza
gharama za uendeshaji ambazo zitatuwezasha kutoa huduma kwa ufanisi Zaidi na
kwa gharama nafuu ili kuwafikia watanzania wengi zaidi na kusogeza huduma
mbambali za kijamii karibu na wananchi zikiwemo huduma za Elimu, Afya na
Mawasiliano. Kazi kubwa kwa wananchi nikulinda huduma hizi na kuzitumia
vizuri kwa shughuli za maendeleo vijijini.”

“Mawasiliano ndio chachu ya maendeleo hivyo tunaamini kwa kutumia umeme wa
jua hata gharama za uendeshaji zitapungua hivyo kuwezesha ktoa huduma zenye
viwango vya juu kwa gharama nafuu kwa watumiaji na wateja wa Airtel nchini
nzima aliongeza Mmbando.”

Kampuni ya Airtel katika kurahisisha mawasiliano nchini inaendelea kufunga
mitambo ya umeme wa sola katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo ya Tanga,
Sumbawanga, Kigoma na mikoa mengine mingi. Mpaka sasa Airtel imefanikiwa
kufunga mitambo minne inayotumia nguvu za jua katika mkoa wa iringa Iringa
vijijini.Mpaka sasa Airtel inaongoza kwa kutoa huduma zenye wigo mpana na
ina vijiji na miji 50 zaidi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents